Iran hivi karibuni imerusha makombora mawili ya balistiki kuelekea kambi ya pamoja ya Marekani na Uingereza katika visiwa vya Diego Garcia katika Bahari ya Hindi, jarida la The Wall Street limeripoti Ijumaa, likinukuu maafisa wa Marekani.
Hakuna kombora lililolenga shabaha, ambayo ni takriban kilomita 4,000 kutoka Iran, lakini shambulizi hilo linaonesha Iran ina makombora ya masafa marefu kuliko iliyodhaniwa awali, ripoti hiyo imesema.
Pentagon imekataa kulizungumzia hilo.
Moja ya makombora lilishindwa kuruka, na jengine lilidukuliwa kutoka meli ya kivita ya Marekani, ingawa haikuwa wazi iwapo kombora lililengwa, limeripoti Jarida.
Diego Garcia ni visiwa vya Chagos nchini Mauritius ambapo kuna moja ya kambi mbili ambazo Uingereza imeiruhusu Marekani kuzitumia kwa ‘operesheni za ulinzi’ wa Iran.
Vikosi vya Marekani vimeweka zana katika kambi, kitovu cha operesheni za Asia, ikiwemo mashambulizi ya Marekani ya mabomu Afghanistan na Iraq.
Uingereza imekubali kuvikabidhi visiwa vya Chagos kwa Mauritius baada ya kuvihodhi tangu miaka ya 60.
Rais wa Marekani Donald Trump ameukosoa vikali uamuzi huo.














