Afrika

Wanajeshi wa Kenya wauawa katika mlipuko wa bomu iliyotegwa

Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri katika wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.

Newstimehub

Newstimehub

16 Julai, 2025

acd60463e7b5c2b90915087eecc7a359f9bc2bbd56d4600c9a37f6aa72363410

Wanajeshi watatu wa Kenya waliuawa Jumanne na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati gari lao lililipuliwa na kilipuzi mashariki mwa kaunti ya Lamu karibu na mpaka na Somalia, jeshi lilisema Jumanne.

Wanajeshi hao walikuwa wakishika doria kando ya barabara kati ya Kiunga na Sankuri wakati gari lao lilipokanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegwa.

“Kwa kusikitisha, wanajeshi watatu mashujaa walikufa kwa majeraha,” Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) lilisema.

Taarifa hiyo ilisema wanajeshi waliojeruhiwa walihamishwa hadi katika vituo maalumu vya kijeshi, na walikuwa wanapokea matibabu, bila kutoa maelezo zaidi.

Ripoti za vyombo vya habari vya ndani zilisema kulikuwa na wanajeshi saba waliojeruhiwa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa uchunguzi umeaznishwa kufuatia tukio hilo.