Afrika Ulimwengu

Wasomali wakamatwa Minneapolis katika msako wa wahamiaji

Operesheni ya serikali kuu yafanyika baada ya matamshi makali ya Trump; viongozi wa jiji walaani.

Newstimehub

Newstimehub

5 Desemba, 2025

84

Maafisa wa serikali kuu Marekani wamewakamata wahamiaji kadhaa mjini Minneapolis, wakiwemo Wasomali watano, katika msako ulioanza Jumatatu. Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Rais Donald Trump kutoa kauli kali dhidi ya wahamiaji wa Kisomali.

Wizara ya Mambo ya Ndani imewataja waliokamatwa kuwa ni wahalifu hatari wenye makosa mbalimbali, huku Meya wa Minneapolis, Jacob Frey, akipinga lugha ya kibaguzi na kuitaka jamii kuonyesha heshima kwa Wasomali. Msako kama huo pia umefanyika New Orleans, na kuzua hofu na maandamano ya wakaazi.