Zaidi ya watu 40 hawajulikani walipo baada ya mashua iliyokuwa imebeba takriban abiria 50 kupinduka katika Jimbo la Sokoto kaskazini magharibi mwa Nigeria, shirika la dharura la nchi hiyo lilisema Jumapili.
“Takriban watu 10 wameokolewa, huku zaidi ya abiria 40 hawajulikani walipo,” Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Dharura (NEMA) lilisema kwenye taarifa.
Kwa mujibu wa taarifa boti hiyo ilikuwa ikielekea Soko la Goronyo.














