Uturuki

Erdogan na Waziri Mkuu wa Uingereza wamejadili kuhusu ndege ya kivita Eurofighter na vita vya Gaza

Ankara inaendeleza mazungumzo kuhusu ununuzi wa ndege za kivita za Eurofighter huku kukiwa na dalili za maendeleo kutoka Ujerumani, wakati Erdogan na Starmer pia wakijadili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na janga la kibinadamu Gaza.

Newstimehub

Newstimehub

22 Julai, 2025

6c5f817e28a58f59f29da6bd93720f5df102972e88771c893c7bdff53e2ec8d8

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer walifanya mazungumzo kwa njia ya simu na kujadili uhusiano wa mataifa mawili, yanayojiri katika kanda, na maendeleo ya mpango Uturuki wa kununua wa ndege za kivita ya aina ya Eurofight, kwa mujibu wa taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais.

Viongozi hao wawili Jumanne walijadili maendeleo katika mpango wa Uturuku wa kununua ndege 40 za Eurofighter, hatua ambayo Ankara inasema itaimarisha ulinzi wa pamoja wa NATO na ushirikiano wa pande mbili na London.

Ndege hiyo iliyotengenezwa kwa pamoja na Uingereza, Ujerumani, Italia na Uhispania, imekuwa mada ya mazungumzo ya miezi kadhaa, huku Uingereza ikiunga mkono mauzo lakini ikikabiliwa na upinzani kutoka kwa Ujerumani.

Wiki iliyopita, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz aliashiria mafanikio yanayoweza kutokea, na hivyo kuongeza matumaini kwamba Berlin inaweza hivi karibuni kuacha pingamizi lake kwa mpango huo.

Upande wa Uturuki pia ulionyesha matumaini kuwa juhudi za kufanya Mkataba wa Biashara Huria wa Uturuki na nchi ya Uingereza kuwa wa kisasa utatoa matokeo mwishoni mwa mwaka.

Gaza imejadiliwa

Kuhusu hali ya Gaza, Erdogan alionya kuwa mzozo wa kibinadamu unazidi kuwa mbaya na kwamba vifo vinavyotokana na njaa vinaendelea.

Alitoa wito wa kuwasilishwa kwa haraka na bila vikwazo misaada ya kibinadamu katika ardhi ya Palestina inayozingirwa.