Uturuki imewasilisha hoja bungeni kutaka kuongezwa kwa muda wa miezi 24 wa uwepo wa wanajeshi wake nchini Libya, ikitaja changamoto za kiusalama na kuendelea kwa sintofahamu ya kisiasa. Ankara inasema uwepo wake unalenga kulinda amani na kuzuia kurejea kwa machafuko, huku ikiunga mkono juhudi za mazungumzo ya kisiasa chini ya Umoja wa Mataifa.
CHANZO: TRT Afrika














