Usalama Afrika Siasa

Maelfu Wafanya Maandamano Kupinga Uhamiaji Haramu Afrika Kusini

Makundi ya wananchi yameandamana nchini Afrika Kusini kupinga uhamiaji haramu wakidai unachangia matatizo ya kiuchumi na kijamii.

Newstimehub

Newstimehub

30 Aprili, 2026

1024x576 cmsv2 a11ef3fc 9b9f 5f9f b860 7305c1e13b82 9741392

Maelfu ya wananchi nchini South Africa wamejitokeza mitaani kufanya maandamano makubwa kupinga uhamiaji haramu, wakieleza kuwa hali hiyo inaathiri ajira, usalama na huduma za kijamii,waandamanaji walikusanyika katika maeneo mbalimbali ya mijini wakibeba mabango na kutoa kauli kali wakitaka serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti wahamiaji wasiokuwa na nyaraka halali. Baadhi yao walidai kuwa wageni wanachukua nafasi za ajira na kuendesha biashara bila kufuata sheria za nchi.

Hata hivyo, mashirika ya haki za binadamu yameonya kuwa maandamano hayo yanaweza kuchochea chuki dhidi ya wageni, hali inayoweza kusababisha vurugu na mashambulizi dhidi ya wahamiaji,serikali ya South Africa imeeleza kuwa inatambua changamoto hiyo na inaendelea kuimarisha sheria za uhamiaji huku ikisisitiza kuwa vitendo vya vurugu havitavumiliwa.

Polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo yenye hatari kubwa ili kuhakikisha maandamano hayo yanafanyika kwa amani bila kusababisha uharibifu wa mali au madhara kwa wananchi,wachambuzi wanasema kuwa suala la uhamiaji haramu nchini humo linahusishwa kwa karibu na changamoto za ukosefu wa ajira na pengo la kiuchumi, jambo linalozidisha mvutano kati ya wenyeji na wageni.

Chanzo:Africanews