Bunge la Zambia limeidhinisha kwa kishindo Muswada wa 7 unaobadilisha vipengele 13 vya katiba vinavyohusiana na uchaguzi, hatua ambayo upinzani unasema itanufaisha Rais Hakainde Hichilema katika uchaguzi wa 2026. Serikali imekanusha madai hayo, ikisisitiza kuwa mabadiliko hayo yanalenga usawa na manufaa ya muda mrefu kwa taifa. Muswada huo sasa unasubiri saini ya rais ili kuwa sheria.
CHANZO: TRT Afrika












