Eritrea imetangaza kujiondoa rasmi kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali za Afrika Mashariki (IGAD), ikilaumu jumuiya hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake na kupoteza mwelekeo. Uamuzi huo, uliotangazwa Disemba 12, 2025, unakuja miaka miwili baada ya Eritrea kurejea IGAD kufuatia kujiondoa awali mwaka 2007. IGAD imesema imesikitishwa na hatua hiyo na kuahidi kuendelea na mazungumzo na Asmara ili kuishawishi ibadili msimamo wake.
CHANZO: TRT Afrika














