Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizoathiriwa na hatua mpya za serikali ya Marekani za kudhibiti uingiaji wa raia wa mataifa kadhaa nchini humo. Hatua hizo zilitangazwa chini ya utawala wa Rais Donald Trump.
Kwa Tanzania, hatua hiyo si marufuku kamili ya kusafiri kwenda Marekani, bali ni udhibiti wa baadhi ya aina za viza, hususan kwa waombaji wapya wa green card na bahati nasibu ya viza (DV Lottery). Marekani imesema uamuzi huo umetokana na changamoto za kiutawala na usalama.
Watanzania wenye viza halali, wanadiplomasia na wakaazi halali wa Marekani bado wanaruhusiwa kuingia nchini humo.
CHANZO: TRT Afrika














