Mshukiwa wa jaribio la kumuua Rais wa Marekani Donald Trump, Cole Allen mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu kujibu mashtaka yanayomkabili kufuatia tukio la ufyatuaji risasi karibu na hafla ya kisiasa mjini Washington.
Allen anakabiliwa na shtaka la kushambulia afisa wa usalama kwa kutumia bunduki baada ya kukamatwa akiwa amejihami kwa bunduki mbili na kisu.
Kwa mujibu wa taarifa za usalama, mshukiwa huyo alikuwa akiishi katika hoteli ya Washington Hilton ambako hafla ya Trump ilikuwa ikifanyika kabla ya kukamatwa baada ya majibizano ya risasi na walinda usalama.
Tukio hilo linaongeza wasiwasi wa kiusalama nchini Marekani kwani linatajwa kuwa jaribio la tatu la kumuua Trump ndani ya kipindi cha miaka miwili.
















