Ulimwengu

Bingwa wa zamani wa ‘Pool Table’ Graeme Dott atupwa jela miaka saba kwa kuwanyanyasa watoto kingono

Raia huyo wa Scotland, ambaye alitwaa ubingwa wa dunia wa ‘Pool Table’ mwaka 2006, amewekwa kwenye orodha ya kudumu ya watuhumiwa wa unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Newstimehub

Newstimehub

29 Septemba, 2026

5515ce0a 8540 45e1 ab21 6e0799d26f8e 1790690382375

Bingwa wa zamani wa mchezo wa ‘Pool Table’ duniani, Graeme Dott, amehukumiwa kifungo cha miaka 7 jela, kwa kosa la unyanyasaji wa watoto kingono.

Dott alipewa hukumu hiyo siku ya Jumanne, baada ya kupatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto wawili.

Raia huyo wa Scotland, ambaye alitwaa ubingwa wa dunia wa ‘Pool Table’ mwaka 2006, amewekwa kwenye orodha ya kudumu ya watuhumiwa wa unyanyasaji wa kingono kwa watoto.