Mabingwa watetezi Ivory Coast na miamba wa soka barani Afrika, Cameroon, walitoka sare ya 1-1 katika mechi ya Kundi F ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyochezwa Jumapili mjini Marrakech.
Ivory Coast walitangulia kupata bao kupitia Amad Diallo dakika ya 51, likiwa bao lake la pili mfululizo kwenye mashindano hayo. Hata hivyo, Cameroon walijibu haraka baada ya dakika tano kupitia shuti kali la Junior Tchamadeu na kusawazisha matokeo.
Kwa matokeo hayo, Cameroon na Ivory Coast sasa wanaongoza Kundi F kwa pamoja wakiwa na pointi nne kila mmoja, huku Msumbiji ikiwafuata kwa pointi tatu.
Diallo alitangazwa mchezaji bora wa mechi kwa mara ya pili mfululizo, akisema ataendelea kupambana na kutoa kiwango bora katika mashindano hayo.
CHANZO: TRT Afrika














