Mamlaka ya Usalama wa Baharini nchini Afrika Kusini (SAMSA) imesema itatoa huduma kuhakikisha usalama na ufanisi kwa meli zinazopita huku ikifuatilia kwa karibu yanayojiri Mashariki ya Kati na athari zake kwa usafiri wa kwenye majini duniani.
Mgogoro unaoendelea kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran tayari umetatiza moja ya njia kuu za baharini, na kulazimisha kampuni za meli kubadilisha njia ya Afrika.
Mkurugenzi Mtendaji wa SAMSA, Dennis Mqadi, amesema wamejiandaa kusaidia meli zote zitakazochagua kupita katika bahari ya Afrika Kusini kwa kuongozwa, kupata taarifa za mara kwa mara, na taarifa za usalama.
Chanzo: TRT Afrika














