Watoto watekwa nyara Nigeria

Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo ya Nigeria linasema wanafunzi 50 kati ya zaidi ya 300 waliotekwa nyara kutoka shule ya Kikatoliki ya Nigeria wametoroka na kuungana na wazazi wao.
24 Novemba, 2025
Taasisi ya Thabo Mbeki yakosoa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Taarifa hiyo inakuja siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuzindua tume itakayochunguza vurugu zilizotokea siku na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, huku akiipa tume hiyo siku 90 za kufanya uchunguzi huo.
24 Novemba, 2025
Gavi, Unicef watia saini mkataba wa kupunguza bei ya chanjo ya malaria

Gavi inakadiria kushuka kwa bei hiyo kutaokoa dola milioni 90, ambazo zinaweza kufadhili dozi milioni 30 zaidi kwa hadi watoto milioni 7 zaidi katika miaka mitano ijayo.
24 Novemba, 2025
Rais wa Nigeria amesema waumini 38 waliotekwa nyara kanisani Nigeria wameokolewa

Rais wa Nigeria Bola Tinubu alisema Jumapili kwamba waumini 38 waliotekwa wakati watu wenye silaha walipovamia ibada ya kanisa wiki jana na kuua watu wawili, wameokolewa.
24 Novemba, 2025

Mkutano wa kilele wa G20 ‘wamalizika vyema’ licha ya kukosekana Marekani baada ya Trump kususia

Afrika kulipa ‘gharama kubwa’ licha ya uhusika mdogo kusababisha mabadiliko ya tabianchi: UN

Tanzania yashutumu vyombo vya habari vya kigeni kwa ‘kuichafua na kuhujumu uchumi wa nchi’

DRC yawaweka jenerali wa jeshi kifungo cha nyumbani kwa ‘kudhoofisha usalama wa nchi’

Azimio la mkutano wa G20 limepitishwa: Msemaji wa rais wa Afrika Kusini
22 Novemba, 2025
Vita vya Sudan: Zaidi ya watoto 20 wanakufa kwa utapiamlo katika mwezi mmoja
Vifo vya watoto hao katika miji chini ya kizuizi ambacho “huzuia kuingia kwa chakula na dawa na kuweka maisha ya maelfu ya raia hatarini.”

22 Novemba, 2025
Mkutano wa viongozi wa G20 unaanza nchini Afrika Kusini
Viongozi wa dunia wakutana kwa siku mbili za mazungumzo katika mkutano wa kwanza wa kilele wa G20 uliofanyika barani Afrika, chini ya mada ya “mshikamano, usawa na uendelevu”.

22 Novemba, 2025
Polisi wa Tanzania waonya dhidi ya maandamano yaliyopangwa ya ‘Siku ya Uhuru’
Wanaharakati na upinzani wametoa wito wa kufanyika maandamano ya amani Desemba 9 ili kuendana na siku ya uhuru wa Tanzania.

22 Novemba, 2025
Guterres anatoa wito kwa G20 kushinikiza kusitishwa mapigano Sudan, kusitisha mtiririko wa silaha
“Tunahitaji amani nchini Sudan,” mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema, akitoa wito “kukomeshwa kwa mtiririko wa silaha na wapiganaji nchini Sudan na vyama vya nje.”

21 Novemba, 2025
Afrika Kusini yakataa kumpokeza Balozi baada ya Marekani kuamua kutoshiriki ‘rasmi’ G20
Afrika Kusini ni nchi ya kwanza ya Afrika kuongoza mkutano wa G20, ikiwa ni urais wa kupokezana kila mwaka tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuwapokeza Marekani.

20 Novemba, 2025
Kiongozi wa harakati za kujitenga ahukumiwa kifungo maisha kwa mashtaka ya ugaidi nchini Nigeria
Mahakama ya Nigeria Alhamisi imemhukumu Nnamdi Kanu, kiongozi wa harakati za kujitenga za Indigenous People of Biafra (IPOB), yaani Watu wa Asili wa Biafra, kifungo cha maisha jela baada ya kumhukumu kwa mashtaka yote saba yanayohusiana na ugaidi.

20 Novemba, 2025
Kamanda wa jeshi la Sudan atoa wito wa kuhamasisha umma dhidi ya RSF
Kamanda mwandamizi wa jeshi la Sudan ametoa wito kwa raia kuitikia ombi la kiongozi wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan wa kutaka waungane nchini nzima dhidi ya wapiganaji wa RSF.

19 Novemba, 2025
Trump kuanza jitihada za kusitisha vita Sudan
Rais wa Marekani Donald Trump alisema Jumatano kuwa ataanza “kufanyia kazi” vita vya Sudan, baada ya Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, aliyekuwa ziarani Marekani, kumwomba kusaidia kumaliza mgogoro huo.

19 Novemba, 2025
Maafisa 2 wa Kenya wamefariki baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa na kundi la al-Shabab
Maafisa wawili wa Kikosi cha Ulinzi wa Mipakani nchini Kenya wamefariki siku ya Jumatano baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa ardhini (IED) na wanamgambo wa al-Shabab wanaotoka Somalia, kwa mujibu wa polisi wa Kenya.

19 Novemba, 2025
Arsenal kusitisha ushirikiano wake na Visit Rwanda
Baada ya miaka nane ya nembo ya Visit Rwanda kupamba bega la jezi za Arsenal, klabu hiyo ilitangaza kuwa itasitisha mkataba wa udhamini na Visit Rwanda ifikapo mwezi Juni 2026.


