Kenya Airways ya Nairobi- Dar es Salaam ililazimika kurudi JKIA kutokana na dharura ya kiafya

Ndege hiyo ya KQ484 ilirudishwa uwanja wa Jomo Kenyatta lakini baada ya itifaki za kiafya kutimizwa iliruhusiwa kuendelea na safari yake saa mbili baadaye.
27 Aprili, 2025
London Marathon: Assefa wa Ethiopia avunja rekodi ya dunia ya mbio za wanawake

Mwanariadha wa Ethiopia Tigst Assefa ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za marathon za wanawake baada ya kushinda mbio za London Marathon kwa saa 2 dakika 15 na sekunde 50 siku ya Jumapili.
27 Aprili, 2025
Wafungwa 4,887 wasamehewa katika sherehe za maadhimisho ya 61 ya Muungano, Tanzania

Hata hivyo kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa, hakuna msamaha kwa watuhumiwa wa hujuma ya uchumi wa nchi, ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya watoto wachanga, ugaidi, biashara ya dawa za kulevya na uhalifu wa mtandaoni.
27 Aprili, 2025
Tanzania yaondoa marufuku ya uagizaji bidhaa kutoka Afrika Kusini, Malawi kuruhusu mazungumzo

Maafisa wa Tanzania wanasema kuwa nchi hizo mbili ziliwasiliana kivyake kutafuta suluhu ya mzozo wa kibiashara kwa njia ya mazungumzo.
27 Aprili, 2025

Uganda yatangaza kumalizika mlipuko wa hivi punde wa Ebola

Viongozi wa Afrika watoa wito kwa walinda amani zaidi Somalia kukabiliana na al-Shabab

DRC na Rwanda zatia saini njia ya kufikia amani katika makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani

Burkina Faso yaipa kampuni ya Urusi Nordgold leseni ya uchimbaji dhahabu

Umeme wakatika Sudan baada ya shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani katika kituo kimoja
25 Aprili, 2025
Mahakama ya Gabon yamthibitisha kiongozi wa kijeshi Nguema mshindi rasmi wa uchaguzi wa urais
Brice Oligui Nguema alipata 94.85% ya kura ikilinganishwa na mpinzani wake mkuu, Alain-Claude By-Nze, aliyepata 3.11%, kulingana na matokeo rasmi ya mwisho.

25 Aprili, 2025
Shirika la Umoja wa Mataifa limefikia watu milioni 4 Sudan lakini linaonya kuhusu njaa kali
Mratibu wa shughuli za dharura anasema Sudan ni nchi pekee ambayo imethibitika kuwa na njaa kali, huku watu milioni 25 wakiwa hawana chakula

25 Aprili, 2025
Uchunguzi wa huduma za mauzo ya viungo nchini Kenya waanza
Kamati huru itafanya ukaguzi wa kina wa huduma zote za upandikizaji wa figo katika hospitali ya Mediheal iliyopo kaunti ya Eldoret katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, baada ya hospitali hiyo kushutumiwa kwa kuhusika na mauzo ya figo.

25 Aprili, 2025
Rwanda kuanza kutibu wagonjwa bila kuhudhuria vituo vya afya
Hospitali zitatumia teknolojia maarufu kama ‘telemedicine,’ mbinu inayotumia teknolojia ya kidijitali kama vile simu za video, programu za simu na majukwaa ya mtandaoni kutoa huduma za afya kwa mbali.

25 Aprili, 2025
Raia wa Rwanda afunguliwa mashtaka Marekani kwa kuhusika na mauaji ya kimbari
Kama inavyodaiwa katika hati ya mashtaka, Faustin Nsabumukunzi aliyeishi Mareknai tangu 2003, alitumia nafasi yake ya uongozi akiwa Rwanda kusimamia ghasia na mauaji ya Watutsi.

25 Aprili, 2025
Dunia yaadhimisha siku ya malaria, nchi 9 Afrika bila malaria
Barani Afrika WHO inasema tangu mwaka wa 2000, zaidi ya wagonjwa wa malaria bilioni 1.7 na vifo milioni 12 vimepukwa katika kanda ya Afrika kutokana na juhudi za kimataifa za afya.

25 Aprili, 2025
Marekani kuwa mwenyeji wa makubaliano kati ya Rwanda na DRC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio atatia saini ‘tamko la kanuni’, siku chache baada ya kutangazwa kusitishwa kwa mapigano kati ya DRC na waasi wa M23 wakati wa mazungumzo ya hivi karibuni yaliyofanywa na Qatar huko Doha.

25 Aprili, 2025
Kenya yaamua tena hisabati kuwa somo la lazima
Haya yanajiri baada ya Wizara ya Elimu kutangaza kuwa masomo ya hesabu hayatakuwa ya lazima tena kwa wanafunzi wa sekondari chini ya Mtaala unaozingatia Umahiri (CBC), mabadiliko makubwa kutoka kwa mfumo ulioondolewa wa elimu.

25 Aprili, 2025
Msumbiji yatangaza kumalizika kwa uasi katika mkoa wenye utajiri wa gesi wa Cabo Delgado
Jeshi linasema limedhibiti kambi za mwisho za mafunzo ambazo bado zilikuwa zinatumiwa na waasi katika mkoa wa kaskazini mwa nchi wa Cabo Delgado.

25 Aprili, 2025
Rais wa Afrika Kusini Ramaphosa kukutana na Trump ‘karibuni’ kusuluhisha matatizo yao
Viongozi hao wawili watajadili kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya serikali ya Trump kusitisha misaada ya fedha kwa Afrika Kusini na kumtimua balozi wao.


