Ushelisheli kufanya uchaguzi wa marudio wa urais baada ya kukosa mshindi wa moja kwa moja

Mpinzani Patrick Herminie alipata 48.8% ya kura, wakati mgombea, Wavel Ramkalawan, alipata 46.4%, kulingana na matokeo rasmi. Mgombea anahitaji kushinda zaidi ya 50% ya kura ili kutangazwa mshindi.
28 Septemba, 2025
Niger yaiambia UNGA Ufaransa lazima ‘ikumbuke na kutambua uhalifu wake’

Lamine Zeine Ali Mahaman, Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ya Kiafrika, katika hotuba yake anaishutumu Ufaransa kwa “kuvuruga” taifa la Sahel kwa kuunga mkono “magaidi” na kuchochea ushindani kati ya Niger na majirani zake.
28 Septemba, 2025
Gambia, Somalia zinakuza sayansi ya uchunguzi kwa ushirikiano na Uturuki

Maafisa wanasema kuanzisha maabara ya DNA iliyoidhinishwa na taifa ni miongoni mwa vipaumbele vya haraka vya Somalia.
28 Septemba, 2025
Utawala wa Trump wabadili vizuizi vya visa kwa Ghana baada ya makubaliano juu ya wahamiaji

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana alisema “habari njema” ilitolewa na maafisa wa Marekani kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
27 Septemba, 2025

Botswana yenye utajiri wa almasi yazindua uraia kwa mpango wa uwekezaji ili kukuza uchumi

Rais wa Madagascar amfuta kazi waziri wa nishati baada ya maandamano kuhusu kukatwa kwa umeme

Hamna watu katika barabara za Madagascar baada ya maandamano ya vurugu

Waziri mkuu wa Sudan aomba UN, jamii ya kimataifa kutangaza RSF kuwa ‘wapiganaji wa kigaidi’

Ethiopia yataka usawa ufikiaji wa Bahari ya Sham na ya Hindi kwa mataifa yote
26 Septemba, 2025
Amri ya kutotoka nje yatangazwa katika mji mkuu wa Madagascar kufuatia maandamano ya fujo
Mamlaka nchini Madagascar siku ya Alhamisi iliweka amri ya kutotoka nje kuanzia jioni hadi alfajiri katika mji mkuu, kufuatia maandamano ya fujo yaliyosababishwa na ukosefu wa umeme na maji wa mara kwa mara, kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa usalama.

26 Septemba, 2025
Urusi na Ethiopia zasaini mpango wa kuanzisha mradi wa nishati ya nyuklia
Urusi na Ethiopia zimesaini mpango wa kuanzisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha nishati ya nyuklia katika nchi hiyo ya Afrika, shirika la habari la TASS limeripoti.

25 Septemba, 2025
Uganda yasaini makubaliano ya kuwapokea kwa muda waomba hifadhi ya kisiasa waliokataliwa Uholanzi
Uholanzi na Uganda wamekubaliana kushirikiana katika suala la kuwapokea waomba hifadhi ya kisiasa waliokataliwa kwa muda, serikali ya Uholanzi ilisema siku ya Alhamisi.

25 Septemba, 2025
Kiongozi wa Al-Shabab miongoni mwa magaidi 24 waliouawa Somalia
Maafisa wa usalama wa Somalia wanasema wameratibu operesheni iliyowalenga viongozi wa al-Shabab na magaidi wengine, na kuwaua magaidi 24.

25 Septemba, 2025
Kenya yatarajia kufikia makubaliano ya biashara na Marekani
Kenya inatafuta kufikia soko la Marekani kwa bidhaa zake za mavazi, nguo na bidhaa za kilimo ikiwa ni pamoja na chai, kahawa na parachichi.

25 Septemba, 2025
Umoja wa Afrika wampongeza Mutharika kwa kushinda uchaguzi wa Malawi
Peter Mutharika amepata ushindi mkubwa dhidi ya Rais aliyekuwa madarakani Lazarus Chakwera, Tume ya Uchaguzi ya Malawi ilitangaza Jumatano.

25 Septemba, 2025
DRC na Rwanda wamekubaliana kuanza kutekeleza hatua za kiusalama mwezi wa Oktoba
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Rwanda wamekubaliana kuanza kutekeleza hatua za kiusalama chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani mwezi ujao, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatano.

24 Septemba, 2025
Tume ya Uchaguzi Malawi yamtangaza Peter Mutharika mshindi wa uchaguzi wa Septemba 16
Aliyekuwa Rais wa Malawi Peter Mutharika amepata kura milioni 3 (aslimia 56.8) kutangazwa rasmi rais-mteule, kwa kumshinda Rais aliye madarakani Lazarus Chakwera, aliyepata kura milioni 1.77 (asilimia 33) katika uchaguzi wa Septemba 16, 2025 .

24 Septemba, 2025
‘Siyo fadhila kwa Afrika’: Hotuba kali ya Rais Ruto wa Kenya UNGA
Rais wa Kenya William Ruto ametoa hotuba kali katika kikao cha 80 cha Umoja wa Mataifa jijini New York, akisema mabadiliko yanahitajika UN, IMF, Benki ya Dunia na taasisi zingine, kwa kuzingatia maslahi ya Afrika kwenye mabadiliko hayo.

24 Septemba, 2025
Uganda : ‘Bobi Wine’ ateuliwa kama mgombea wa urais 2026
Aliwania wadhifa wa juu nchini mwaka 2021 lakini akashindwa na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni.



