Afrika

Guterres: Tanzania ni kielelezo cha amani Afrika na duniani

Tanzania imeendelea kuwa mfano wa amani na mshikamano wa kijamii.

Newstimehub

Newstimehub

15 Desemba, 2025

4897dca47792863b1ebb6aa9394a2d4f475683a6689ef34fd06c8a16d18f79a9

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameisifu Tanzania akiitaja kuwa kielelezo cha amani barani Afrika na duniani, akisema taifa hilo linaonekana kimataifa kama mfano wa kuigwa katika mshikamano wa kijamii. Akizungumza baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka Tanzania, Guterres alikiri kuwa sifa hiyo ilipitia majaribio wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, lakini akaeleza kufurahishwa na jinsi nchi ilivyovuka changamoto hizo. Alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa na kusema UN iko tayari kusaidia juhudi za kuchunguza na kudumisha amani. Kauli yake inakuja wakati baadhi ya nchi za Magharibi zikitathmini upya uhusiano wao na Tanzania, huku taifa hilo likiendelea kuwa miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa barani Afrika.

CHANZO: TRT Afrika