Jamhuri ya Congo inajiandaa kufanya uchaguzi mkuu tarehe 15 Machi 2026 huku rais wa sasa Denis Sassou Nguesso akiwa mgombea wa chama tawala cha Parti Congolais du Travail.
Sassou Nguesso, mwenye umri wa miaka 82, anachuana na wagombea wengine sita katika uchaguzi huo. Hata hivyo, vyama viwili vya upinzani vimesusia mchakato huo kwa madai kuwa haukidhi vigezo vya uwazi na haki.

Kiongozi huyo alichukua madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 1979 wakati wa mfumo wa chama kimoja. Baada ya kushindwa uchaguzi wa 1992, alirejea madarakani mwaka 1997 kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe na tangu wakati huo ameendelea kushinda chaguzi mbalimbali.
Iwapo atashinda tena, Sassou Nguesso ataendelea kuiongoza nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta kwa muhula mwingine.
CHANZO: TRT Afrika














