Umoja wa Mataifa umesema raia wasiopungua 104, wakiwemo watoto 43, wameuawa katika mashambulizi ya droni eneo la Kordofan nchini Sudan tangu Disemba 4. Mashambulizi hayo yamelenga maeneo ya kiraia ikiwemo hospitali na shule, huku pande zinazozozana zikiendelea kulaumiana kuhusu matumizi ya ndege zisizo na rubani.
CHANZO: TRT Afrika













