Afrika

Eritrea yajiondoa IGAD

Ikumbukwe kwamba, hapo awali, Eritrea ilisitisha uanchama wake ndani ya IGAD mnamo mwezi Aprili, 2007.

Newstimehub

Newstimehub

12 Desemba, 2025

f4a925b2869f4e9e4786fd3532f250ef5ed33cdacb01e1148b49f1eeda8483d5

Eritrea imejiondoa kwenye Jumuiya ya maendeleo ya serikali za nchi za Afrika mashariki, maarufu kama IGAD.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Disemba 12, 2025 na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo, Eritrea imeafikia uamuzi huo baada ya kuona, kuwa kwa kipindi cha miaka 20, Jumuiya ya IGAD imeshindwa kufikia malengo na matakwa ya watu waishio kwenye kanda hiyo.

Ikumbukwe kwamba, hapo awali, Eritrea ilisitisha uanchama wake ndani ya IGAD mnamo mwezi Aprili, 2007.

Hata hivyo, iliamua kurudi tena mwezi Juni 2023, ikiwa na matumaini kuwa IGAD itashughulikia maoni ya Eritrea ya kutaka maboresho ndani ya Jumuiya hiyo.

Eritrea imesisitiza kuwa Jumuiya ya IGAD imeendelea kupoteza dira na mwelekeo wake.

Kwa upande wake, IGAD imesema kuwa imesikitishwa uamuzi wa Eritrea, ikisema kuwa itaendelea kuzungumza na serikali ya Eritrea ili iweze kubadili maamuzi yake.