Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino, amesema shirikisho hilo linaweza kuiondolea Urusi adhabu ya kutoshiriki mashindano ya kimataifa. Infantino alieleza kuwa hatua hiyo ya kusimamishwa imekuwa ikipandikiza chuki badala ya kuleta suluhu.
Kauli hiyo imepingwa vikali na Waziri wa Michezo wa Ukraine, Matvii Bidnyi, ambaye amesema maoni ya Infantino hayana uwajibikaji.
Urusi ilisimamishwa kushiriki mashindano yote ya FIFA na UEFA tangu Februari 2022, baada ya kuivamia Ukraine.
CHANZO: TRT Afrika














