Ghana na European Union wamesaini makubaliano yao ya kwanza rasmi ya ushirikiano wa kijeshi, hatua inayolenga kuimarisha usalama katika ukanda wa Afrika Magharibi.
Makubaliano hayo yanakuja wakati ambapo eneo hilo linakabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya makundi ya wanajihadi, hali inayotishia utulivu wa nchi kadhaa jirani. Ghana imejipambanua kama ngome muhimu ya kulinda usalama wa kikanda dhidi ya vitisho hivyo.
Kupitia ushirikiano huo, pande zote zinatarajia kuboresha mafunzo ya kijeshi, kubadilishana taarifa za kiintelijensia, na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na ugaidi.
Chanzo: Africanews














