Michezo

Hatma ya Mohamed Salah Liverpool yatiliwa shaka kabla na baada ya CAN Morocco

“Hakuna tatizo lolote la kutatua kati yangu na Salah.”
— Arne Slot, kocha wa Liverpool

Newstimehub

Newstimehub

15 Desemba, 2025

142 1

Mustakabali wa nyota wa Misri Mohamed Salah katika klabu ya Liverpool unaendelea kuwa kitendawili huku akijiandaa kuiongoza Misri katika Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) litakalofanyika Morocco. Salah aliingia kipindi cha pili na kutoa pasi ya bao katika ushindi wa Liverpool wa mabao 2-0 dhidi ya Brighton, lakini bado tetesi zinaendelea kufuatia kauli zake kali wiki iliyopita. Kocha Arne Slot amepuuza uvumi huo akisisitiza kuwa hakuna mgogoro wowote, licha ya Salah kukaa benchi katika mechi kadhaa mfululizo, ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Inter Milan. Kauli ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kwamba “alifanywa kafara” imezidisha minong’ono ya uwezekano wa kuondoka kwake Liverpool wakati wa dirisha la usajili wa majira ya baridi.

CHANZO: TRT Afrika