Watu wenye silaha wameua takriban watu 30 katika shambulio la msikiti kaskazini magharibi mwa Nigeria, hayo ni kwa mujibu wa mkazi na mbunge wa eneo hilo, na kuongeza idadi ya waliokufa kutoka 13.
“Watu wenye silaha,” makundi ya uhalifu kama wanavyojulikana, wameshambulia msikiti uliopo katika mji wa Unguwar Mantau siku ya Jumanne, katika jimbo la Katsina.
“Waumini tisa waliuliwa hapo kwa hapo na wengine wengi walikufa baadae. Idadi za hivi punde za waliopoteza maisha ni 32,” amesema Nura Musa, mkazi wa eneo hilo siku ya Jumatano.














