Ulimwengu Siasa

Indonesia Yaunga Mkono Utawala Mpya wa Iran

Indonesia yasema itaheshimu uongozi mpya wa Mojtaba Khamenei baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei.

Newstimehub

Newstimehub

10 Mechi, 2026

460

Serikali ya Indonesia imesema itaheshimu utawala mpya wa Iran unaoongozwa na Mojtaba Khamenei.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, Yvonne Mewengkang, alisema serikali yao inafuatilia kwa karibu maendeleo ya kisiasa nchini Iran kufuatia uteuzi huo.

Uongozi wa Mojtaba unakuja baada ya kifo cha aliyekuwa kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, aliyeripotiwa kuuawa katika mashambulizi yaliyodaiwa kufanywa na United States na Israel.

Mbali na Indonesia, nchi nyingine zilizotambua utawala huo mpya ni pamoja na Russia, Iraq, Oman, Azerbaijan na Belarus.

Mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yameongeza mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati, yakiripotiwa kusababisha vifo vya watu takribani 1,300.

CHANZO: TRT Afrika