Jeshi la Mali linasema limetibua shambulio katika kambi ya jeshi, ‘kuwakata makali’ magaidi 13

‘Jaribio la wapiganaji magaidi’ kutaka kuingia katika kambi ya jeshi ya Timbuktu lilitibuliwa, na hali sasa imetulia na ‘imedhibitiwa,’ Jeshi la Mali lilisema

Newstimehub

Newstimehub

2 Juni, 2025

30bcf7b4219c7a5b7081e71afe0f6883de90e2fef5b7c97e22521ebd110c6a6a

Siku ya Jumatatu jeshI la Mali lilisema limefanikiwa kutibuwa “jaribio la magaidi” la kutaka kuvamia kambi ya kijeshi ya Timbuktu kaskazini mwa Mali.

Magaidi kumi na tatu “walikatwa makali,” na silaha, magari na vitu vingine vilipatikana, taarifa hiyo ya jeshi ilisema.

Ilisema kuwa hali kwa sasa “imedhibitiwa” na juhudi za kuwasaka zinaendelea kote mjini Timbuktu.

Taarifa hiyo haikutaja kundi la kigaidi ambalo limehusika na jaribio hilo, lakini wapiganaji wote wenye uhusiano na makundi ya ISIS (Daesh) na al-Qaeda wamewahi kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo siku za nyuma.

Haya yamejiri siku moja baada ya shambulio la magaidi kulenga kambi ya kijeshi ya Boulkessi katikati mwa eneo la Douentza.