Afrika

Kesi ya Joseph Kony yaendelea ICC bila mwenyewe kuwepo

Mahakama ya ICC imeanza kusikiliza kesi ya Joseph Kony, kiongozi wa kundi la Lord’s Resistance Army, LRA.

Newstimehub

Newstimehub

10 Septemba, 2025

db2348adb309f0ff7a671dd562b9e7deb1468c75b26169a828e8d447fdb8cd27

Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC inaendelea kusikiliza kesi dhidi ya Joseph Kony, raia wa Uganda aliyeongoza kikundi cha uasi nchini Uganda.

Kony alidai kuwa alitaka kuongoza Uganda kupitia amri kumi za Mungu.

Kulingana na Umoja wa Mataifa shughuli za LRA ziliua takriban watu 100,000 na kuwalazimisha takriban milioni 2.5 barani Afrika kuhama makwao kati ya 1986 na 2009.
ICC iliamuru akamatwe 2005 lakini hadi sasa wakati kesi yake inaanza kusikilizwa bila ya yeye mwenyewe kuwepo.

Kundi la LRA lilifurushwa kutoka Uganda mwaka 2005, na waasi hao wakaingia katika lililokuwa eneo la Sudan na hatimaye kuweka kambi katika mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

89ad8277faac3a52516722922188a7b4cc1ba60acd47f78d09ae8ad1d592a42a 1

Baadaye walihamia Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako inafahamika walijihusisha na ujangili na uchimbaji madini haramu.

Kulikuwa na majaribio ya serikali ya Uganda kufanya makubaliano ya amani na Kony, lakini mazungumzo yalivurugika mwaka 2008 kwa sababu kiongozi huyo wa LRA alitaka kuhakikishiwa usalama wake na washirika wake.