Kiongozi wa mpito wa Madagascar ametangaza kuvunjwa kwa serikali nzima pamoja na kumfuta kazi waziri mkuu katika hatua inayolenga kupanga upya uongozi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, uamuzi huo umefanywa ili kuunda serikali mpya itakayoweza kushughulikia changamoto za kiuchumi na kijamii zinazolikabili taifa hilo la visiwa katika Bahari ya Hindi.
Hatua hiyo imezua mjadala katika duru za kisiasa nchini humo, huku wachambuzi wakisema inaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko mapya katika uongozi wa serikali.
Chanzo: TRT Afrika














