Kundi la waasi la M23 linasema limewakamata mamia ya wanajeshi wa Burundi wakati wa mashambulio ya hivi karibuni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, madai ambayo Reuters hayakuweza kuthibitisha.
Wiki iliopita M23 iliingia mji wa kimkakati wa Uvira karibu na mpaka wa Burundi, chini ya wiki moja baada ya marais wa DRC na Rwanda kukutana Washington na Rais wa Marekani Donald Trump na kuthibitisha dhamira kwa makubaliano ya amani yanayojulikana kama Makubaliano ya Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema Jumamosi kuwa hatua za Rwanda mashariki mwa DRC yamekiuka Makubaliano ya Washington na kuapa “kuchukua hatua kuhakikisha ahadi walizoweka kwa rais zinatimizwa.”
Pamoja na kuwa Rwanda inakabiliwa na shutuma za kuunga mkono M23, inakanusha madai hayo na kulaumu vikosi vya Congo na Burundi kuanzisha tena mapigano.
Rais wa Burundi aonya kuhusu kulipiza kisasa iwapo M23 itashambulia vikosi vyake
M23 imesema “wanajeshi wa Burundi waliokamatwa” watasindikizwa kurejea “nyumbani.”
Pamoja na kuwa hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa Burundi siku ya Jumatatu, ambyo imekuwa na vikosi vyake mashariki mwa DRC kwa miaka kadhaa, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye amewahi kuwaonya M23 dhidi ya kuanzisha vita na nchi yake.













