Mvua kubwa imenyesha Gaza kwa siku ya pili mfululizo, ikifunika mamia ya hema katika kambi za wakimbizi na kuwaacha maelfu ya Wapalestina bila makazi, joto au chakula. Idara ya ulinzi wa raia imesema imeondoa hema kadhaa katika Rafah baada ya kuzama kabisa, huku ikionya kuwa zaidi ya familia 250,000 ziko hatarini kutokana na baridi na maji ya mvua. Dhoruba inatarajiwa kuendelea hadi Ijumaa, na kusababisha kuongezeka kwa mateso ya wakazi waliokimbia makazi yao kutokana na vita vya Israel. Serikali ya Gaza inasema takribani hema 300,000 yanahitajika, huku gharama ya kujenga upya eneo hilo ikikadiriwa kufikia dola bilioni 70.
CHANZO: TRT Afrika














