Watalii wawili wa Kituruki pamoja na dereva wao wa Kietiopia wameuawa kwa risasi na watu wenye silaha katika eneo la vijijini karibu na mji wa Tum, Kusini Magharibi mwa Ethiopia. Tukio hilo lilitokea Januari 12, na balozi wa Türkiye mjini Addis Ababa, Berk Baran, amethibitisha vifo hivyo.
Wakati wa shambulio, raia wanne wa Kituruki walikuwa wakisafiri kwa magari mawili. Waliokuwa kwenye gari la mbele waliokoka bila madhara na waliripoti tukio hilo kwa ubalozi. Miili ya waliouawa tayari imepelekwa Addis Ababa na inatarajiwa kusafirishwa Istanbul kwa ndege ya Turkish Airlines.
Balozi Baran amesema serikali ya Ethiopia imechukua hatua za haraka, ikihusisha wizara na vikosi vya usalama katika uchunguzi na uratibu wa miili na manusura. Amepongeza ushirikiano wa mamlaka za Ethiopia na kutoa pole kwa familia za marehemu.
CHANZO: TRT Afrika














