Rwanda imeilaumu DRC na Burundi kwa kukiuka mkataba wa amani wa Washington baada ya mashambulizi yanayodaiwa kufanywa katika vijiji vya mpakani kwa ndege za kivita. Kigali imesema haitawajibishwa kwa machafuko ya Kivu Kusini, ikitaja kuwa majeshi ya DRC, Burundi na wanamgambo wanavunja makubaliano ya usitishwaji wa mapigano. Tuhuma hizi zimeibuka siku mbili baada ya Rais Tshisekedi kuiweka Rwanda lawamani, huku Rwanda ikidai Burundi imekusanya wapiganaji 20,000 kuisaidia DRC katika Minembwe.
CHANZO: TRT Afrika














