Afrika

Mchakato wa kujisajili kwa wapiga kura Kenya kuanza tena Septemba 29

Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) imetangaza kuanza tena kwa mchakato wa kusajili wapiga kura kote nchini.

Newstimehub

Newstimehub

29 Agosti, 2025

76cb01be573a09cfff7a4570843fcb112199f372be1631489346080d2f6f7e9c

Tume hiyo ya IEBC ilieleza kuwa itaanza mchakato wa usajili Septemba 29, huku maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 yakipamba moto.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Alhamisi, Tume imesema inalenga kupata wapiga kura wapya waliotimiza umri wa miaka 18, na raia wa Kenya ambao hawakuwa wamejisajili awali, pamoja na wale wanaotaka kuhamisha vituo vya kupiga kura.