Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Yousouf, amelaani vikali jaribio la mapinduzi nchini Benin, akilitaja kama ukiukaji mkubwa wa kanuni za AU na kuingilia mchakato wa kisiasa. Yousouf aliwataka wanajeshi waliohusika kuacha mara moja vitendo vyao na kurejea kambini bila kuchelewa, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu Katiba ya Benin. AU imeeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa mapinduzi barani Afrika, ikionya kuwa yanaathiri utulivu wa bara na kudhoofisha imani ya wananchi kwa taasisi za umma. ECOWAS pia ililaani jaribio hilo, huku serikali ya Benin ikisema kuwa jeshi limeudhibiti na Rais Patrice Talon yuko salama.
CHANZO: TRT Afrika














