Mkuu wa mtihani wa kitaifa wa kujiunga na vyuo vikuu Korea Kusini, Suneung, amejiuzulu baada ya kukosolewa vikali kwa kuweka maswali magumu kupita kiasi, ambayo wanafunzi walilinganisha na kusoma maandishi ya kale. Oh Seung-geol alikiri kuwa kiwango cha ugumu “hakikuwa sahihi” na kwamba mtihani haukutimiza vigezo. Maswali tata kuhusu falsafa ya Immanuel Kant na maneno ya michezo ya mtandaoni ndiyo yaliyozua mkanganyiko mkubwa.
CHANZO: BBC NEWS














