Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir, ametoa wito wa utulivu na umoja huku maandamano yaliyopangwa kufanyika Disemba 9 yakiendelea kuzua wasiwasi. Ametaka Watanzania waepuke kauli na matangazo ya chuki, na badala yake waunge mkono mikakati ya mazungumzo na maridhiano. Mufti amesema taasisi za dini zimeanza mazungumzo chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa BAKWATA kupitia Taasisi ya Tanzania Interfaith Partnership (TIP), yakilenga kuimarisha amani na kulinda maisha na mali za wananchi. Ametoa mwito kwa wananchi kuwa watulivu na kuepuka uchochezi, hasa katika mitandao ya kijamii, akisisitiza kwamba dini zisiruhusiwe kuchochea maandamano yanayoweza kuleta mgogoro.
CHANZO: TRT Afrika














