Idadi ya wakimbizi wa Kongo nchini Burundi imeongezeka kufuatia mapigano mashariki mwa DR Congo, hususan baada ya M23 kuteka mji wa Uvira. Serikali ya Burundi inasema zaidi ya watu 76,000 wamekimbilia nchini humo ndani ya siku chache, huku Umoja wa Mataifa ukionya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu na kuomba fedha za dharura ili kukidhi mahitaji ya msingi ya wakimbizi hao kwa miezi minne ijayo.
CHANZO: BBC NEWS














