Afrika

Mwanasiasa Adolf Hitler ashinda kwa mara ya 5 mfululizo Namibia

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 59 anasema yeye ni tofauti kabisa na dikteta huyo wa Ujerumani, na anapenda atambuliwe kwa jina lake la asili

Newstimehub

Newstimehub

28 Novemba, 2025

5e3179dd4f55c1a2b80a36736f72147c7685daa885b25c95cf9e0cfe9d125563

Mwanasiasa wa Namibia aliyepewa jina la dikteta wa Ujerumani Adolf Hitler amepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kulingana na matokeo rasmi yaliyotangazwa siku ya Alhamisi.

Adolf Hitler Uunona, ambaye kwa sasa anapenda kufahamika kama Adolf Uunona, alishinda tena nafasi yake katika eneo bunge la kaskazini la Ompundja kanda ya Oshana kwa kupata kura 1,275, huku mpinzani wake pekee, Isak Akawa, akipata kura 148.

Uunona, ambaye hana uhusiano wowote na dikteta wa Ujerumani, aliwania kwa tiketi ya chama tawala cha nchi hiyo ya Kusini Magharibi cha SWAPO, huku Akawa akiwa na chama cha IPC.

Uunona amekuwa katika nafasi hiyo ya udiwani katika nchi iliyo koloni la zamani la Ujerumani tangu 2004 na, mapema wiki hii, alitangaza kuwa angependa kutambulika rasmi kama Adolf Uunona kuanzia sasa.

Alinukuliwa na vyombo vya habari vya sehemu hiyo akisema hataki tena kutambuliwa kwa jina lake la kuzaliwa kwa kuwa matendo yake na mtazamo ni tofauti na kiongozi huyo wa Kinazi wa Ujerumani, ambaye anasema hata hamfahamu vizuri.