Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amewataka wananchi kutunza na kutumia kwa uangalifu chakula walichonacho kufuatia kuchelewa kwa msimu wa mvua katika baadhi ya maeneo ya nchi. Akizungumza Dodoma, alisema utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) unaonyesha mvua za chini ya wastani hadi wastani katika mikoa kadhaa, hali inayoweza kuathiri uzalishaji wa mazao. Nchemba alisisitiza kuwa licha ya kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula kitaifa, tahadhari na matumizi sahihi ni muhimu. Aidha, aliwahimiza wakulima kuandaa mashamba mapema, kutumia pembejeo zinazofaa na kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo.
CHANZO: TRT Afrika













