Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) linadai kuwa baadhi ya wachezaji wa DR Congo, wakiwemo Aaron Wan-Bissaka na Axel Tuanzebe, hawakuwa na sifa za kucheza kutokana na masuala ya uraia pacha. DR Congo imekanusha madai hayo, ikiyataja kama jaribio la kushinda “kwa mlango wa nyuma,” huku FIFA ikisubiriwa kutoa uamuzi wake.
CHANZO: BBC NEWS











