Polisi nchini Kenya wamemkamata Festus Omwamba anayeshukiwa kuhusika katika mpango wa kuwalaghai Wakenya kwa ahadi za kazi nchini Urusi. Inadaiwa kuwa baadhi ya waliokubali ofa hizo walipelekwa kushiriki vita vya Ukraine badala ya kufanya kazi walizoahidiwa.
Mshukiwa huyo alikamatwa katika mji wa Moyale baada ya kuripotiwa kujificha kufuatia malalamiko ya familia zilizodai ndugu zao kupotea au kuathirika vitani. Polisi wanasema uchunguzi unaendelea ili kubaini watu wengine waliohusika katika mtandao huo.
CHANZO: TRT Afrika














