Afrika

Tanzania yamuachilia Boniface Mwangi

Boniface Mwangi mwanaharakati wa Kenya na mwenzake wa Uganda Agather Atuhaire walikamatwa na mamlaka za Tanzania siku ya Jumatatu walipokwenda nchini humo wakitaka kuhudhuria kesi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu.

Newstimehub

Newstimehub

22 Mei, 2025

2025 05 21t121441z 1 lynxmpel4k0lt rtroptp 3 tanzania politics 1 2

Serikali ya Kenya imethibitisha kuachiwa kwa mwanaharakati wa nchi hiyo Boniface Mwangi. Awali Boniface alikuwa anashilikiwa nchini Tanzania baada ya kuingia nchini humo kwa lengo la kutaka kuhudhuria kesi ya Tundu Lissu, kiongozi wa chama cha upinzani Chadema.

Kwa mujibu wa ofisi ya Mambo ya Nje ya Kenya, na vyombo vya habari vya Kenya, Boniface alisafirishwa kwa njia ya barabara na kupatikana katika mji wa Ukunda uliopo Pwani ya Kenya, takriban kilomita 30 kutoka mji wa Mombasa.