Tanzania imeadhimisha miaka 64 ya Uhuru katika mazingira ya tahadhari ya kiusalama, huku serikali ikiwashauri wananchi kubaki majumbani kufuatia wito wa maandamano yanayopinga utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan. Miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam ilibaki tulivu bila shughuli nyingi. Serikali imesema maandamano si halali, wakati mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa kuheshimu haki za binadamu. Rais Samia ametangaza wito wa maridhiano, ingawa haijulikani kama upinzani utakubali kushiriki mazungumzo hayo.
CHANZO: TRT Afrika














