Afrika

Tanzania: Yanga yatwaa taji la Ngao ya Jamii ikiifunga Simba 1-0

Bao pekee la ‘Wananchi’ lilipatikana katika dakika 53 ya mchezo, kupitia kwa mchezaji wao nyota, Pacome Zouzoua, na hivyo kuifanya Simba kupoteza mchezo wao wa sita mfululizo katika michezo tofauti, mbele ya mahasimu wao wa jadi.

Newstimehub

Newstimehub

17 Septemba, 2025

e1f29c1f821bdede175a14c02fbc202318b2f50712292bb7d7b25911f6ed6d95

Simba Sports Club imeendeleza ‘uteja’ wake mbele ya mahasimu wao Young Africans, baada ya kufungwa bao 1-0, katika mchezo wa Ngao ya Jamii, uliofanyika Septemba 16, 2025, katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.