Amri hiyo imetolewa baada ya kuzuka kwa maandamano ya kupinga shughuli za uchaguzi.
Taarifa ya kutotoka nje imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.
Hapo awali shirika linalofuatilia masuala ya huduma za mitandao duniani, Netblocks limeeleza kuwepo kwa kutatizika kwa huduma za mitandao nchini Tanzania siku ya Uchaguzi Mkuu, ikiwa thibitisho la taarifa za kutokuwepo kwa huduma hizo kama ilivyo kawaida.













