Waziri Mkuu wa Thailand Anutin Charnvirakul amesema nchi yake haitaki vurugu lakini italinda uhuru wake, baada ya Thailand kufanya mashambulizi ya anga kufuatia shambulio lililoua mwanajeshi mmoja. Cambodia imekanusha kuanzisha mapigano huku pande zote zikituhumiana kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano.
CHANZO: BBC NEWS














