Donald Trump ametoa kauli kali dhidi ya NATO, akiutaja kama “dhaifu japo unaonekana kuwa na nguvu” (paper tiger).
Katika mahojiano na gazeti la Daily Telegraph, Trump alisema kwa muda mrefu amekuwa hana imani na uwezo wa muungano huo wa kijeshi.
Aliongeza kuwa hata Vladimir Putin anatambua udhaifu huo, akisema hali hiyo inaathiri taswira ya NATO kimataifa.
Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu nafasi ya Marekani ndani ya muungano huo muhimu wa kiusalama.
CHANZO: TRT Afrika














