Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Afrika Kusini haitoalikwa katika mkutano wa mwaka ujao wa G20 huko Miami, akiendeleza uhasama wake wa kidiplomasia zaidi.
Trump alitaja siku ya Jumatano kile alichokieleza kuwa “ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu” uliofanyiwa wakulima wazungu, na Afrika Kusini kukataa kuwapokeza urais wa G20 Marekani mwishoni mwa kongamano la mwaka huu.
“Afrika Kusini imeonehsa kwa Dunia si nchi ambayo inafaa kuwa wanachama popote pale,” Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.
Serikali ya Trump haikuwa na mwakilishi katika mkutano wa G20 wa mwaka huu, uliomalizika jijini Johannesburg, akisema vipaumbele vya Afrika Kusini, ikiwemo ushirikiano kuhusu biashara na mabadiliko ya tabianchi, ambao ulikuwa kinyume na sera zake.
Kujibu hilo, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alikataa kuupokeza rasmi urais wa G20 kwa mwenyeji wa mwakani, Marekani, kama ilivyo utamaduni.














