Afrika

Upinzani Kenya yatishia kumrudisha Rais Ruto ICC

Vitisho vya upinzani kumrudisha Rais Ruto katika Mahakama ya Kimatifa ya Uhalifu vinakuja baada ya rais huyo kutoa amri kwa polisi kuwapiga risasi watu wenye kuvunja sheria wakati wa maandamano.

Newstimehub

Newstimehub

14 Julai, 2025

e58f5178f46eb3696fe3e553be4e719af47a7ee052d5009dd30412d69cd9349c

Aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga amemuonya Rais William Ruto kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inaweza kurejea nchini kutokana na maandamano ya hivi majuzi.

Katika kikao na waandishi wa habari, alidai kuwa matamshi na maagizo ya kizembe ambayo rais anayatoa, haswa wakati huu ambapo mvutano wa kisiasa unafikia kilele, yamevutia hisia za jumuiya ya kimataifa, hasa ICC.

“Sitashangaa kuona ICC imerejea, kwa sababu mara ya mwisho walikuwa wanakufuata, mashahidi hawakuwepo. Watu hao si wajinga, na safari hii wanaweza kufanya uchunguzi wao vizuri na kurejea,” Maraga alisema.

Onyo hilo la Maraga linakuja siku chache baada ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kufichua kwamba ameandaa timu ya kukusanya ushahidi dhidi ya Rais William Ruto katika harakati za kuandaa kesi dhidi yake katika mahakama ya ICC.

Hapo awali Ruto ametoa amri kwa polisi kuchukua hatua madhubuti katika kukabiliana na watu wenye kuvunja sheria wakati wa maandamano.

Kulingana na kiongozi huyo, watu hao wapigwe risasi miguuni kwa minajili ya kudhibitiwa na si kuuwawa.